NJIA YA KIANGLIKANA: ALAMA ZA SAFARI TUNAYOISAFIRI PAMOJA
Maandiko hayo yanatokea baada ya mafautano ya mikutano ya muda ya zaidi ya miaka mine. Kati ya mikutano hio, viongozi wa kanisa, wanatheologia na waalimu za kitheologia wamejitoa mno watafakari juu ya mambo ya kiAnglikana, yaani maana, maisha na matendo ya KiAnglikana. Wanafikiri mambo hayo huitwa “Njia ya KiAnglikana” na kuwekwa kama msingi kwa kuelezea Uanglikana kwa maaskofu, wachungaji na walei.
Karatasi hiyo haiwezi kuelezea kila kitu cha Uanglikana, lakini inaweka alama zile zinazoonyeshea waAnglikana jinsi ya kutembea pamoja na wengine na kushirikiana nao wanapojitambua na kumfuata Yesu Kristo.
Safari hii bado inaendeala kwa kuwa mazingira na hali tofauti hubadilishabadilisha maana ya Uanglikana. Katika historia ya kanisa aina tofauti za kiAnglikana zimeonekana mpaka sasa, na bado zipo kwenye ushirika wa KiAnglikana ya sasa hivi. Lakini waAnglikana wa kila aina hushirikiana vifaa ya hali moja vinavyowaunganisha ulimwenguni kote yaani “vifungo vya upendo” (bonds of affection). Alama zinazofuata chini huandikwa ili maana na utumishi wa kiAnglikana ujulikane vizuri zaidi na pia waAnglikana wote wafundishwe mno na kuwezeshwa kwa kumhudumia Mungu ujumbe wake hapa duniani.
Njia ya Kianglikana ni njia moja inayoonyensha jinsi waKristo wanavyoishi katika Kanisa Takatifu, Katholiko na Apostoliko lililojengwa juu ya msingi wa Bwana wetu Yesu Kristo. Njia hiyo
Kila mahali tofauti ulimwenguni kote WaAnglikana katika maisha yao na matendo yao wanamshuhudia Bwana wetu aliyefanywa mwanadamu, akasulibiwa na akafufuka. Pia WaAnglikana wote huwezeshwa na Roho Mtakatifu kwa kazi hiyo.
Pamoja na Wakristo wote wenzao Waanglikana wanajitoa kuombea na kusubiri kwa hamu ufalme ujao wa Mungu.
1 Sisi WaAnglikana husikiliza sauti ya Mungu anayeishi katika Maandiko Matakatifu yaliyopokezanywa katika akili na mazoeo. Sisi tunasoma Biblia, kila mmoja peke yake au pamoja:
2. Katika maisha yetu yote tunapenda mno Maandiko Matakatifu kila neno. Pia tunathamani Maandiko Matakatifu yanavyotuonyesha jinsi ya kumfuata Yesu kila mahali na kila hali. Sisi tunaomba na kuimba sifa zake katika ibada zetu na nyimbo zetu. Orodha za masomo zinatufungulia baraka na neema za Maandiko Matakatifu kwa maisha yetu ya hapa duniani.
3. Tukijishusha na kujiweka chini ya mamlaka ya Maandiko Matakatifu sisi hufungiliwa mioyo yetu na masikio yetu na kusikiliza vilevile. Maandiko Matakatifu yametunzwa kama urithi wetu wa kiRoho, kwa mfano, katika Imani za Kanisa la kale, Kitabu cha Sala kwa Watu Wote, na taratibu za Kanisa la KiAnglikana, yaani,
4. Tukihuburi na kumshudhudia Neno liliofanywa mwandamu, yaani, Yesu, pia tunawathamani waliosoma kwa taratibu na unagalifu Maandiko Matakatifu tangu siku zile za kwanza mpaka sasa. Sisi pia tunaomba tuwe hivyo tukiishi katika imani yetu, yaani, watu
Kila siku sisi twaona kwamba hali mpya zinaomba shauri mpya na majibu mapya yanayotokea kutoka maisha ya kiRoho na imani inayohusika na Maandiko Matakatifu.
5. Mawasiliano yetu na Mungu husaidiwa na jinsi tunavyokutana na Mungu Baba, Mwana na Roho Mtakatifu katika Neno na Sakramenti. Mazoeo hayo husaidia na kuongeza jinsi tunavyomjua Mungu na pia tunavyoshirikiana na waKristo wenzetu.
6. Kama waAnglikana tunamsifu Mungu, yaani Utatu Mtakatifu, tukisali pamoja na kupanga ibada zetu katika uhuru na umoja. Tukitubu na kumshukuru Mungu tunajitoa na kumhudumia Mungu hapa duniani.
7. Katika ibada zetu na sala zetu sisi hujaribu kuungunisha matokeo yenye maana kutoka zamani zilizopita pamoja na desturi na mira tofauti za jamii zetu mbalimbali za sasa hivi.
8.Sisi na jamii zetu tumesharibika na dhambi. Hata hivyo tunajua tunavyoomba msaada wa Mungu na kusamehewa naye. Tunajua pia tunavyoishi katika neema na jinsi ya kutayarisha maisha yetu yawe safi mbele yake Mungu. Sisi tunavyosamehewa na Kristo na kuwezeshwa tuwe imara katika neno na sakramenti hutumwa tuingilie ulimwengu katika nguvu ya Roho Mtakatifu.
9. Kwenye madayosisi na majimbo yetu yaliyoendeshwa na maaskofu na synodi sisi tumefurahi mno miito mbalimbali ya wote waliobatizwa. Kama ilivyoandikwa kwenye taratibu za kuweka wakfu maaskofu, mashemasi na makasisi, vyeo hivi vitatu hufanya wachungaji wahudumu ili waite watu wote wa Mungu na kuwapangia na kuendeshea kazi zao kama zilivyojulikana na kufanikiwa.
10. Sisi waAnglikana tunathamani mno tunavyoishi pamoja duniani kote. Tunamweka Askofu Mkuu wa Canterbury awe mtu anayeonyesha alamu wa umoja wetu na kushirikiana pamoja na Uaskofu wa Canterbury. Pia tunashika vifaa vitatu kwa ushirikiano:
Mikutano hiyo mitatu pamoja na Askofu Mkuu wa Canterbury mwenyewe huunganisha Ushirika wa KiAnglikana katika dunia bila kuweka mamlaka yote sehemu moja peke: upendo na vifungo vyake husaidia kazi zao vizuri zaidi.
11. Pia inabidi tukubali jinsi jamii za kimisionari na kimataifa (kwa mfano, UMAKI) jinsi zinavyowasaidia kujenga umoja katika ushirika wetu. Maisha tunayoyashirikiana katika ushirika wetu pia husaidiwa na kamati mbalimbali, jamii tofauti, kazi tunazozishirikiana na jirani zetu na vifungu vya undugu ( kwa mfano, kati ya madayosisi).
12. Sisi waAnglikana twaitwa tujitoe kwa ujumbe wa Mungu hapa duniani. Sisi tunafanya hivyo ktk kazi mbalimbali:
Tunapotoa ujumbe mahali petu mbalimbali sisi tunamhudumia na kumshuhudia Yesu Kristo Mwokozi wetu aliyesulibiwa na kufufuka. Tunamshangilia pia Mungu alivyotusamehe na kutupa sisi uzima wa milele tukichungulia ushuhuda wenye gharama kubwa,imani na uaminifu uliotolewa na wanawake, wanaume na watoto wa ushirika letu leo na tangu zamani.
13. Pia tunakumbuka kwamba kazi zetu kwa ujumbe wa Mungu na maisha yetu ya kiKristo hazifai na hazitoshi. Zimechafuliwa na makosa mbalimbali:
Tukikumbuka makosa hayo tunaomba kujishusha na kubadilika ili tumfuate Mungu kwa upole mpya na kushirikiana habari njema kwa furaha katika maneno yetu na matendo yetu tunavyojitoa.
14. Tukisimama imara katika Kristo twashirikiana na watu wote wenye moyo safi katika kazi za kujengea amani, haki, upendo na msamaha ya Mungu. Tunajua shida kubwa ziko mbele ya sisi, kwa mfano:
Hatutakaa kimya mbele yao. Tutahubiri unabii kwa kuvunja falsafa na visiasa vya udanganyifu na uharibifu. Pia tutaendelaa na mazoeo yetu mazuri kwa kuwasaidia watu ka njia za elimu, kiafya na uradhi.
15. Tukiwasiliana na watu wa dini tofauti, tutamshuhudia Bwana wetu Yesu Kristo katika amani, upole, akili na heshima.
16. Sisi WaAnglikana tunaobatizwa katika Kristo tunashirikiana na WaKristo wenzetu wa madhehebu mbalimbali katika ujumbe wa Mungu. Tuna hamu sana kwa kuwasiliana vizuri na WaKristo wa madhehebu tofauti. Mazoeo yetu katholiko pamoja na yalivyotengenezwa ni baraka kwa mawasiliano wetu na madhehebu mengine. Tunawasiliana nayo kwa sababu tunaamini na kutumaini kwamba WaKristo wote watashika umoja ule ambao Mungu ameshawapangia ili watu wote wa dunia wasikilize injili ya Bwana wetu Yesu Kristo na kuiamini.
TEAC Anglican Way Consultation
Singapore
May 2007
Kiswahili translation by Revd Dr Fergus King,
June 2007
To whom any errors should be attributed….